SportPesa SUPER CUP: YANGA NJE, FAINALI KENYA TUPU -MAHASIMU GOR v AFC!

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Juni 5

Robo Fainali

AFC Leopards 1 Singida United 1 [Penati 5-4]

Yanga 0 Tusker FC 0 [Penati 4-2]

Jumanne Juni 6

Simba 0 Nakuru All Stars 0 [Penati 4-5]

Gor Mahia 2 Jang’ombe Boys 0

Alhamisi Juni 8

Nusu Fainali

AFC Leopards 0 Yanga 0 [Penati 4-2]

Gor Mahia 2 Nakuru All Stars 0

Jumapili Juni 11

Fainali

Saa 10 Jioni

AFC Leopards v Gor Mahia

+++++++++++++++++++++++++++++++++

SPORTPESA-SUPERCUPYANGA, Timu pekee ya Tanzania iliyokuwa imebaki kwenye SpoertPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, Leo wametupwa nje baada ya kushindwa Nusu Fainali kwa Penati 4-2 na AFC Leopards ya Kenya.

Fainali ya michuano hii itakuwa kati ya Timu za Kenya tupu ambazo ni Mahasimu Wakuu huko Kenya, AFC Leopards na Gor Mahia ambao kwenye Nusu Fainali nyingine walipiga Timu nyingine ya Kenya Nakuru All Stars 2-0.

Mechi ya Yanga na AFC Leopards ilimalizika 0-0 kwenye Dakika 90 na kuja Mikwaju ya Penati Tano Tano ambapo Kipa wa AFC, Dennis Shika, aliokoa Penati 2 zilizopigwa na Said Musa na Said Juma ‘Makapu’ na Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, kuokoa Penati ya Ingotsi.

Wafungaji wa Penati 2 za Yanga ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Obrey Chirwa wakati 4 za AFC kupachikwa na Bernard Mango, Allan Katerega, Duncan Otieno na Dennis Shika.

Habari MotoMotoZ