SportPesa SUPER CUP: LEO NUSU FAINALI, YANGA KUIBEBA TANZANIA?

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Juni 5
SPORTPESA-SUPERCUPRobo Fainali
AFC Leopards 1 Singida United 1 [Penati 5-4]
Yanga 0 Tusker FC 0 [Penati 4-2]
Jumanne Juni 6
Simba 0 Nakuru All Stars 0 [Penati 4-5]
Gor Mahia 2 Jang’ombe Boys 0
Alhamisi Juni 8
Nusu Fainali
Saa 8 Mchana AFC Leopards v Yanga
Saa 10 na Robo Jioni Gor Mahia v Nakuru All Stars
Jumapili Juni 11
Fainali
Saa 10 Jioni
AFC Leopards/Yanga v Gor Mahia/Nakuru All Stars
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MICHUANO ya kugombea SportPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, itaendelea Leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa Mechi 2 za Nusu Fainali.

Yanga, Timu pekee ya Tanzania iliyobaki Mashindanoni baada Simba na Jang'ombe Boys kutupwa nje, watacheza na AFC Leopards ya Kenya na kufuatia Mechi nyingine kati ya Timu za Kenya pekee Gor Mahia itakapocheza na Nakuru All Stars.
Washindi wa Mechi hizi watavaana kwenye Fainali hapo Jumapili Juni 11.
 
 
 

Habari MotoMotoZ