SportPesa SUPER CUP: DUUU..SIMBA CHALIII! SASA YANGA MOJA DHIDI KENYA 3!

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Juni 5

Robo Fainali

AFC Leopards 1 Singida United 1 [Penati 5-4]SPORTPESA-SUPERCUP

Yanga 0 Tusker FC 0 [Penati 4-2]

Jumanne Juni 6

Simba 0 Nakuru All Stars 0 [Penati 4-5]

Gor Mahia 2 Jang’ombe Boys 0

Alhamisi Juni 8

Nusu Fainali

Saa 8 Mchana AFC Leopards v Yanga

Saa 10 na Robo Jioni Gor Mahia v Nakuru All Stars

Jumapili Juni 11

Fainali

Saa 10 Jioni

AFC Leopards/Yanga v Gor Mahia/Nakuru All Stars

+++++++++++++++++++++++++++++++++

MICHUANO ya kugombea SpoertPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, imeeendelea Leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Timu za Kenya, Gor Mahia na Nakuru All Stars, kutawala huku Wabongo Simba na Jang’ombe Boys wakitupwa nje.

Matokeo haya yameiacha Tanzania ikiwa na mtetezi moja tu ambae ni Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga ambao Jana walitinga Nusu Fainali na watacheza na AFC Leopards hapo Alhamisi.

Nusu Fainali nyingine itakayochezwa Siku hiyo hiyo ni kati ya Gor Mahia na Nakuru All Stars.

Mapema Leo, Gor Mahia iliichapa Jang’ombe Boys 2-0 huku Bao zote zikipigwa Medie Kegere za Kipindi cha Pili moja likiwa la Penati.

Mechi hiyo ikafuatiwa na Simba na Nakuru All Stars na kwenda 0-0 hadi Dakika 90 na Simba kupigwa nje kwa Penati 5-4.

Nakuru All Stars walifunga Penati zao zote 5 zikimpenya Kipa Daniel Agyei huku wao wakifunga 4 na mkosaji wa hiyo moja yao ni ile iliyopigwa na Kipa huyo kutoka Ghana ikiwa ni Penati ya Pili.  

Habari MotoMotoZ