SportPesa SUPER CUP: YANGA KUIVAA AFC LEOPARDS NUSU FAINALI!

>JUMANNE SIMBA v NAKURU ALL STARS, GOR v JANG’OMBE!

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Juni 5SPORTPESA-SUPERCUP

Robo Fainali

AFC Leopards 1 Singida United 1 [Penati 5-4]

Yanga 0 Tusker FC 0 [Penati 4-2]

Jumanne Juni 6

Saa 8 Mchana Simba v Nakuru All Stars

Saa 10 na Robo Jioni Gor Mahia v Jang’ombe Boys

Alhamisi Juni 8

Nusu Fainali

Saa 8 Mchana AFC Leopards v Yanga

Saa 10 na Robo Jioni Mshindi RF3 v Mshibdi RF 4

Jumapili Juni 11

Fainali

Saa 10 Jioni

+++++++++++++++++++++++++++++++++

MICHUANO ya kugombea SpoertPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, imeaanza Leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, na AFC Leopards ya Kenya kutinga Nusu Fainali wote wakipita kwa Matuta baada ya Sare ndani ya Dakika 90.

Kwenye Mechi ya Kwanza hii Leo, Timu Mpya ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, Singida United, inayoongozwa na Kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm, ilitangulia kufunga Bao Dakika ya 20 kupitia Pro wao kutoka Zimbabwe Kutinyu Tafadzwa.

Lakini AFC Leopards walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Vincent Oburu.

Hadi Dakika 90 kwisha Gemu ilibaki 1-1 na ikaja Tombola ya Mikwaju Mitano ya Penati ambapo AFC Leopards walifuzu kwa Penati 5-4.

Baada ya Mechi hii wakaingia Yanga ambao walitoka 0-0 na Tusker FC ya Kenya lakini kufuzu kwa Penati 4-2 ambazo za Yanga, waliochezesha Chipukizi wengi,  zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Obrey Chirwa, Maka Edward Mwakalukwa na Said Mussa.

Tusker FC walifunga Penati 2 wakati moja ikiokolewa na Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na nyingine kutoka nje baada kuparaza Posti.

Kwenye Nusu Fainali Yanga watacheza na Tusker FC.

Habari MotoMotoZ