CAF CHAMPIONZ LIGI: LEO NI NGAYA NA YANGA ESTADIO DE MORONI, COMORO!

=JANA ZIMAMOTO YA ZENJI 2 FERROVIARIO 1!
CAF-CC-17MASHINDANO MAKUBWA ya Klabu Barani Afrika yalianza Jana kwa Klabu za Tanzania huko Amaan Stadium Zanzibar, wakati Zimamoto ilipoichapa Ferroviario Beira ya Mozambique 2-1 na Leo Yanga wako Ugenini huko Comoro kuivaa Ngaya Club.
Leo pia huko Amaan Stadium Zanzibar, KVZ itacheza na Le Messager Ngozi ya Burundi katika Mechi ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Timu nyingine ya Tanzania ambayo ipo kwenye michuano ya Klabu Afrika ni Azam FC ambayo inaanza Raundi ya ya Timu 32 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Mshindi kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Msafara wa Yanga kuelekea Visiwa vya Comoro ulitua Jana huko Moroni ukiwa na Watu 30 wakiwemo Wachezaji 20, Benchi la Ufundi Mtu 8 na Maafisa Wawili wakiongozwa na Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa.
Lakini Kikosi cha Timu hiyo kitawakosa Straika wa Zimbabwe Donald Ngoma na pia Malimi Busungu ambao ni Wagonjwa.
Wengine ambao hawamo Kikosini ni Mchezaji wa Togo Vincent Boussou, Pat Ngonyani na Kipa Beno Kakolanya huku Vincent Andrew akiachwa kwa kuwa Kifungoni kutokana na kulambwa Kadi za Njano 3 Msimu uliopita kwenye Mashindano ya CAF.
Msimu uliopita Yanga walitolewa Raundi ya Pili ya Mashindano haya na El Ahly ya Egypt kwa Jumla ya Bao 3-2 katika Mechi 2 na kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho walikofika Hatua ya Makundi na kumaliza Nafasi ya 4 kwenye Kundi B.
Ikiwa Yanga wataitoa Ngaya kwenye Raundi hii ya Awali watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda ambazo Jana zilitoka 0-0 huko Zambia.
Endapo Yanga watavuka tena hatua hiyo watatua Hatua ya Makundi.
Nao Zimamoto, wakivuka Raundi ya Awali, watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi wa Mechi ya Barrack Young Controllers ya Liberia na Stade Malien ya Mali.
==================
Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.
Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.
Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.
Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.        
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Awali
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Februari 10
KCC – Uganda 1 Primeiro 0
JS Saoura 1 Enugu Rangers – Nigeria 1
JumamosiFebruaria 11
Zanaco – Zambia 0 APR - Rwanda 0
Royal Leopards – Swaziland 0 AS Vita – Congo DR 1
Cnaps Sports – Madagascar 2 Township Rollers – Botswana 1
Zimamoto – Zanzibar 2 Ferroviario Beira – Mozambique 1
Tusker – Kenya 1 AS Port Louis -Mauritius 1
Royal Club du Kadiogo – Burkina Faso 3 Diables Noirs - Congo 0
AS Real de Bamako – Mali 0 Rivers United – Nigeria 0
SS Saint-Louisienne – Reunion 2 Bidvest Wits - South Africa 1
FC Johansens - Sierra Leone 1 Fath Union Sport de Rabat - Morocco 1
Côte d'Or – Seychelles 0 Kedus Giorgis - Ethiopia 2     
Lioli Football Club – Lesotho 0 CAPS United FC - Zimbabwe 0   
AS Tanda - Ivory Coast 3 AS-FAN - Niger 0
CF Mounana – Gabon 2 Vitalo FC - Burundi 0    
US Gorée – Senegal 0 Horoya Athlétique Club - Guinea 0       
Jumapili Februari 12
15:00 Ngaya Club – Comoros v Young Africans - Tanzania    
17:00 Coton Sport FC – Cameroon v Atlabara FC - South Sudan     
17:00 Gambia Ports Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast
17:00 All Stars FC – Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya     
17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon
19:00 Barrack Young Controllers FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali   
19:30 Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan