TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI: ZIMAMOTO YA ZENJI JUMAMOSI NA FERROVIARIO, JUMAPILI YANGA WAPO COMORO!

>>JUMAPILI NI ZENJI, KVZ NA LE MESSAGER NGOZI YA BURUNDI - KOMBE LA SHIRIKISHO!

CAF-CC-17MASHINDANO makubwa ya Klabu Barani Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, yanaanza hii Leo kwa Raundi ya Awali lakini Klabu za Tanzania zitaingia dimbani Jumamosi na Jumapili.

Hapo Jumamosi, huko Amaan Stadium Zanzibar, Zimamoto itacheza na Ferroviario Beira ya Mozambique na Jumapili, Yanga wako Ugenini huko Comoro kuivaa Ngaya Club.

Jumapili, huko Amaan Stadium Zanzibar, KVZ itacheza na Le Messager Ngozi ya Burundi katika Mechi ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.

Timu nyingine ya TTanzania ambayo ipo kwenye michuano ya Klabu Afrika ni Azam FC ambayo inaanza Raundi ya ya Timu 32 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Mshindi kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Ikiwa Yanga watavuka Raundi hii ya Awali watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda.

Endapo Yanga watavuka tena hatua hiyo watatua Hatua ya Makundi.

Nao Zimamoto, wakivuka Raundi ya Awali, watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi wa Mechi ya Barrack Young Controllers ya Liberia na Stade Malien ya Mali.

Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.

Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.

Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.        

CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Awali

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Februari 10

KCC – Uganda 1 Primeiro 0

2100 JS Saoura v Enugu Rangers – Nigeria

JumamosiFebruaria 11

1600 Zanaco – Zambia v APR - Rwanda

1600 Royal Leopards – Swaziland v AS Vita – Congo DR

1630 Cnaps Sports – Madagascar v Township Rollers – Botswana

1630 Zimamoto – Zanzibar v Ferroviario Beira – Mozambique

1700 Tusker – Kenya v AS Port Louis -Mauritius

1700 Royal Club du Kadiogo – Burkina Faso v Diables Noirs - Congo

1700 AS Real de Bamako – Mali v Rivers United – Nigeria

17:00 SS Saint-Louisienne – Reunion v Bidvest Wits - South Africa 

17:00 FC Johansens - Sierra Leone v Fath Union Sport de Rabat - Morocco

17:00 Côte d'Or – Seychelles v Kedus Giorgis - Ethiopia       

17:00 Lioli Football Club – Lesotho v CAPS United FC - Zimbabwe   

17:00 AS Tanda - Ivory Coast v AS-FAN - Niger

17:30 CF Mounana – Gabon v Vitalo FC - Burundi      

20:00 US Gorée – Senegal v Horoya Athlétique Club - Guinea         

Jumapili Februari 12

15:00 Ngaya Club – Comoros v Young Africans - Tanzania    

17:00 Coton Sport FC – Cameroon v Atlabara FC - South Sudan     

17:00 Gambia Ports Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast

17:00 All Stars FC – Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya     

17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon

19:00 Barrack Young Controllers FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali   

19:30 Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan