AZAM SPORTS FEDERATION CUP – RAUNDI YA 6: RATIBA YATOKA, MABINGWA YANGA NA KILUVYA, AZAM-MTIBWA, SIMBA-LYON!

AZAM-ASFC-CUP>IPO DABI YA MBEYA!

Raundi ya ya Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), imetolewa na Mechi zake zitaanza Februari 24.

Raundi hii inashirikisha Jumla ya Timu 16 na Washindi wake kutinga Robo Fainali ambayo itafanyika Droo maalum ili kupanga Mechi zake.

Februari 24 zipo Mechi 4 na Raundi hiyo itaendelea na kumalizika Tarehe 7 Machi wakati Mabingwa Watetezi Yanga wakicheza Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Kiluvya.

Mechi za Februari 24 ni kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar huko Azam Complex, Chamazi na nyingine ni Kagera Sugar v Stand United, Mighty Elephant v Ndanda FC na Madini v JKT Ruvu.

Wakati Azam FC wakicheza Nyumbani kwao Februari 24 na Mtibwa Sugar, Simba watacheza pia Nyumbani hapo Machi Mosi na African Lyon.

Katika Raundi hii, Mechi ngumu ni ile Dabi ya Mbeya kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City na zile za Timu za VPL pekee, Mbao FC na Toto Africans na Kagera Sugar na Stand United.

AZAM SPORTS FEDERATION CUP – RAUNDI YA 5

Ratiba:

ASFC-RAUNDI YA 6