VPL: MABINGWA, VINARA YANGA WAPAA ZAIDI JUU KILELENI, WAIFUMUA STAND 4 MTUNGI!

VPL-DTB-SITVINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Mabingwa Watetezi Yanga Leo wakiwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wameichapa Stand United 4-0.

Ushindi huu umewaweka juu zaidi kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 21 wakifuata Simba wenye Pointi 44 kwa Mechi 20.

Bao za Yanga hii Leo zilifungwa na Donald Ngoma, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Kesho Jumamosi zipo Mechi 2 za VPL Kati ya Mbeya City na JKT Ruvu na nyingine ni Maji Maji FC na Simba.

VIKOSI:

YANGA: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan [Andrew Vincent ‘Dante’], Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma [Juma Mahadhi], Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima [Emmanuel Martin]

STAND UNITED: Sebastain Stanley [Mohammed Makaka], Jacob Massawe, Erick Mulilo, Adeyum Ahmed, Revocatus Richard, Ibrahim Job, Abdulaziz Makame, Adam Salamba, Frank Khamis [Amri Kiemba], Abasalim Chidiebele [Aaron Lulambo], Suleiman Kassim

REFA: Suleiman Kiungani [Morogoro]

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokeo:

Ijumaa Februari 3

Yanga 4 Stand United 0

Jumamosi Februari 4

Mbeya City v JKT Ruvu

Maji Maji FC v Simba

Jumatatu Februari 5

Toto Africans v Ruvu Shooting

Jumanne Februari 7

Azam FC v Ndanda FC

Jumatano Februari 8

Tanzania Prisons v JKT Ruvu