BINGWA AFRIKA MAMELODI SUNDOWN WAGOMEWA NA YANGA, SIMBA ILA AZAM FC KUDUNDA NAO!

>>MKWASA KATIBU MKUU YANGA!

TFF-MKWASAVIGOGO wa Tanzania, Yanga na Simba, zote zimegoma kucheza na Klabu ya Afrika Kusini Mamelodi Sundown ambao ndio Mabingwa wa Afrika wanaozuru Tanzania kwa Mechi za kushiriki Kampeni ya kupiga Vita Ujangili, ‘Linda Tembo Wetu’.

Mamelodi Sundown walitakiwa kucheza na Simba Jumatano kisha Yanga Ijumaa zote zikiwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam lakini Vigogo hao wote wamekataa mwaliko wa kucheza nao wakitaja ushiriki wao VPL, Ligi Kuu Vodacom.

Simba Jumamosi wako huko Songea kucheza na Majimaji FC wakati Yanga Jumapili wako Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Stand United.

Hivi sasa kuna vita kali ndani ya VPL baada ya Juzi Yanga kuwang’oa Simba kileleni mwa VPL walikokuwa wakiongoza tangu Agosti.VPL-JAN29

Sasa Mamelodi Sundowns wanatarajiwa kucheza na Azam FC huko Azam Complez, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.

WAKATI HUO HUO, Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wamethibitisha kuwa Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga.

Mkwasa, ambae alikuwa Kocha wa Yanga na kisha kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, anashika wadhifa huo uliokuwa ukikukaimiwa na Baraka Deusdedit ambae anarejea kuwa Mkuu wa Idara ya Fedha hapo Yanga.

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba

Jumamosi Februari 4

Mbeya City v JKT Ruvu

Majimaji FC v Simba

Azam FC v Ndanda FC

Jumapili Februari 5

Mbao FC v Mtibwa Sugar

Yanga v Stand United

Jumatatu Februari 6

Toto Africans v Ruvu Shooting

Jumatano Februari 8

Tanzania Prisons v JKT Ruvu