VPL: MABINGWA YANGA WAREJEA PENYEWE, WASHIKA HATAMU!

VPL-DTB-SITMABINGWA WATETEZI wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga Leo wameinyuka Mwadui FC 2-0 kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushika uongozi wa Ligi hiyo.

Bao zote za Yanga zilifungwa Kipindi cha Pili na Mzambia Obrey Chirwa alieingizwa Kipindi hicho kutoka Benchi kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima.

Bao la Kwanza kwa Yanga lilifungwa Dakika ya 69 baada ya Kipa wa Mwadui FC Shaaban Kado kutema Shuti la Simon Msuva na VPL-JAN29Chirwa kuutokea Mpira na kuukwamisha wavuni.

Chirwa tena akapiga Bao la Pili Dakika ya 83 baada ya kumalizia Krosi ya Mwinyi Haji iliyoparazwa kwa Kichwa na Thabani Kamusoko.

Ushindi huu umewaweka Mabingwa Yanga kileleni mwa VPL baada ya kuing’oa Simba walioshikilia kilele tangu Agosti.

Yanga sasa wana Pointi 46 na Simba 45 huku zote zikiwa zimecheza Mechi 20 kila moja.

VIKOSI:

YANGA: Deo Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe [Said Juma ‘Makapu’, 81’], Haruna Niyonzima [Obrey Chirwa, 68;’], Deus Kaseke [Emmanuel Martin, 52’]

MWADUI FC: Shaaban Kado, Nassor Masoud 'Chollo', Malika Ndeule, Yassin Mustafa [David Luhende, 81’], Iddi Mobby, Razack Khalfan, Hassan Kabunda [Salum Kanoni, 89’], Awadh Juma, Paul Nonga, Salim Khamis [Joseph Kimwaga, 86’], Abdallah Seseme

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokdeo:

Jumapili Januari 29

Yanga 2 Mwadui FC 0

Jumatatu Januari 30

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

JKT Ruvu v Stand United