MAPINDUZI CUP: YANGA NI KISHINDO, YAFUMUA 6!

>JUMANNE NI SIMBA-KVZ, JANG’OMBE BOYS-URA!

AMAAN-STADIUM-17MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga wameanza Mechi zao za Kundi B la Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, kwa kishindo kikubwa kwa kuifumua Jamhuri ya Pemba Bao 6-0.

Hadi Mapumziko Yanga 4 Jamhuri 0 kwa Bao za Simon Msuva, Dakika za 19 na 40, na Donald Ngoma, Dakika za 23 na 37.

Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao nyingine 2 kupitia Thaban Kamusuko na Juma Mahadhi.

Mechi inayofuata kwa Yanga kwenye Mapinduzi Cup ni Jumatano dhidi ya Zimamoto ambayo mapema Leo ilifungwa 1-0 na Azam FC katika Mechi iliyochezwa mapema Leo.

+++++++++++++++++

MAKUNDI:

KUNDI A

-Simba

-Taifa Jang;ombe

-Jang’ombe Boys

-KVZ

-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B

-Yanga

-Azam FC

-Jamhuri

-Zimamoto

+++++++++++++++++

Jumanne Januari 3, zipo Mechi 2 za Kundi A wakati Jang'ombe Boys wakicheza na Mabingwa Watetezi URA kuanzia Saa 10 Jioni na KVZ kuivaa Simba Saa 2 na Nusu Usiku.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys vs URA (Saa 10:00 jioni)

KVZ vs Simba (Saa 2:30 usiku)

Januari 4, 2017

Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)

Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017

KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.