MAPINDUZI CUP: LEO SIMBA DIMBANI NA TAIFA JANG’OMBE, KESHO YANGA NA JAMHURI!

AMAAN-STADIUM-17MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ya kuenzi Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba ambayo yalianza Juzi huko Amaan Stadium, Zanzibar kwa Mechi moja ya Kundi A, Leo tena yapo dimbani kwa Mechi nyingine mbili za Kundi A ambazo pia zitachezwa Uwanja wa Amaan.

Juzi Usiku, Timu pinzani huko Zanzibar zilipambana na Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0.

Leo, Saa 10 Jioni ni KVZ na URA ya Uganda, ambao ndio Mabingwa Watetezi, na Usiku Saa 2 na Nusu ni Simba na Taifa Jang’ombe.

+++++++++++++++++

MAKUNDI:

KUNDI A

-Simba

-Taifa Jang;ombe

-Jang’ombe Boys

-KVZ

-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B

-Yanga

-Azam FC

-Jamhuri

-Zimamoto

+++++++++++++++++

Mechi za Kundi B zitaanza Kesho Januari 2, kwa Azam FC kucheza na Zimamoto kuanzia Saa 10 Jioni na Yanga kuivaa Jamhuri Saa 2 na Nusu Usiku.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

**Mechi zote kuchezwa Amaan Stadium, Zanzibar

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ vs URA (Saa 10:00 jioni)

Simba vs Taifa Jang'ombe (Saa 2:30 usiku)

Januari 2, 2017

Azam vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni

Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku)

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys vs URA (Saa 10:00 jioni)

KVZ vs Simba (Saa 2:30 usiku)

Januari 4, 2017

Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)

Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017

KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.