VPL: MABINGWA YANGA WAIDUNDA NDANDA, SASA POINTI 1 NYUMA YA VINARA SIMBA!

>>ALHAMISI SIMBA-RUVU SHOOTING, AZAM-PRISONS!

VPL-LOGO-MURUAMABINGWA Watetezi Yanga Leo Jijini Dar es Salaam wameitandika Ndanda FC Ba0 4-0 katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, na kujikita zaidi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba.

Simba wana Pointi 41 kwa Mechi 17 na Yanga Pointi 40 kwa Mechi 18.

Hadi Mapumziko, Yanga walikuwa mbele 3-0 kwa Bao 2 za Mzimbabwe Donald Ngoma, Dakika za 4 na 21, na Amissi Tambwe, 25, na Kipindi cha Pili kuongeza moja kupitia Vincent Bossou, 89.

Kipigo hiki kimeitupa Ndanda FC Nafasi ya 13 wakiwa na Pointi 19 kwa Mechi 18.

Katika Mechi nyingine iliyochezwa Leo Mtibwa Sugar waliiwasha Majimaji FC 1-0 huko Manungu, Morogoro.

Matokeo hayo yameipandisha Mtibwa Sugar hadi Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 30 kwa Mechi 18 na kuiacha Majimaji FC Nafasi ya 14.

Nafasi ya 4 inashikiliwa na Kagera Sugar wenye Pointi 28 kwa Mechi 17 na wa 5 ni Azam FC wenye Pointi 27 kwa Mechi 17.

Alhamisi zipo mechi 2 za VPL na moja ipo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Ruvu Shooting na Simba na nyingine ni pia Jijini Dar es Salaam huko Azam Complex kati ya Azam FC na Tanzania Prisons.

VPL - Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Desemba 26

Ruvu Shooting 2 Tanzania Prisons 0

Jumatano Desemba 28

Yanga 4 Ndanda FC 0

Mtibwa Sugar 1 Majimaji FC 0

Alhamisi Desemba 29

Ruvu Shooting v Simba [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]

Azam FC v Tanzania Prisons [Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam]

Jumamosi Desemba 31

Mwadui FC v Kagera Sugar [Mwadui Complex, Mwadui]

African Lyon v JKT Ruvu [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]

Mbeya City v Mbao FC [Sokoine, Mbeya]

Jumapili Januari 1

Toto African v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]