VPL DIMBANI LEO HUKO MABATINI, JUMATANO MABINGWA YANGA TAIFA NA NDANDA!

VPL-LOGO-MURUAVPL, Ligi Kuu Vodacom, inaendelea Leo kwa Mechi moja huko Mabatini, Mlandizi ambako Ruvu Shooting watacheza na Tanzania Prisons.

Mechi hii inazikutanisha Prisons ambayo ipo Nafasi ya 7 ikiwa na Pointi 22 na Ruvu Shooting ikiwa Nafasi ya 9 na ina Pointi 20.

VPL itaendelea tena Jumatano Desemba 28 kwa Mechi 2 ambako huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Mabingwa Watetezi Yanga kucheza na Ndanda FC na huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar watacheza na Majimaji FC.VPL-DES24

Alhamisi pia zipo Mechi 2 kati ya Ruvu Shooting na Simba na nyingine ni Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons.

Hadi sasa, Simba wapo kileleni wakiwa na Pointi 41, Yanga ni wa Pili wenye Pointi 37 na Kagera Sugar wanakamata Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 28,Azam Fc wanafuatia wakiwa na Pointi 27 sawa na Mtibwa Sugar.

VPL

Ligi Kuu Vodacom

Jumatatu Desemba 26

Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandazi]

Jumatano Desemba 28

Yanga v Ndanda FC [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

Mtibwa Sugar v Majimaji FC [Manungu, Manungu]

Alhamisi Desemba 29

Ruvu Shooting v Simba [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]

Azam FC v Tanzania Prisons [Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam]

Jumamosi Desemba 31

Mwadui FC v Kagera Sugar [Mwadui Complex, Mwadui]

African Lyon v JKT Ruvu [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]

Mbeya City v Mbao FC [Sokoine, Mbeya]

Jumapili Januari 1

Toto African v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

Matokeo:

Jumamosi Desemba 24

Mbeya City 0 Toto Africans 0 [Sokoine, Mbeya]

Kagera Sugar 1 Stand United 0 [Kaitaba, Bukoba]

Ndanda FC 0 Mtibwa Sugar 2 [Nangwanda, Mtwara]

Simba 1 JKT Ruvu 0 [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Majimaji FC 1 Azam FC 1 [Majimaji, Songea]

Mwadui FC 1 Mbao FC 0 [Mwadui Complex, Mwadui]